Harmonize ampachika mimba mpenzi wake wa kizungu (Picha)

Harmonize sasa anatarajia kuwa mzazi wakati wowote, staa huyo wa Wasafi amempachika mimba mpenzi wake wa kizuri miezi michache baada ya mapenzi yake na Jacqueline Wolper kuvunjika.

Akiongea kwenye kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV, Wolper alisema kuwa uhusiano wake wa kimapenzi na Harmonize uliisha miezi mitatu iliyopita.

download latest music    

“Nyie mnajua sisi tumeachana juzi? Tumeacha miezi mitatu iliyopita kabla hata ya wimbo wake Niambie haujatoka. Sisi wenyewe tuliamua kukaa kimya kwa sababu kuachana sio kugombana kuna kesho mnaweza kushirikiana katika mambo mengine ya kibiashara,” Wolper alisema.

Wolper na Harmonize

Harmonize aliharakisha kuingia katika uhusiano nyingine baada ya kukosana na Wolper, kwa sasa mpenzi wake ni mzungu.

Hit maker huyo wa ‘Happy Birthday’ alitangaza kwa Instagram kuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake wa kizungu.

Mrembo wa kizungu wa Harmonize

“Mnh! nawaza huu mchanganyiko wa damu ya kimakonde na ya kizungu sijui itatuletea mwana gani… asa nikiona kakomwe hapo, kananistua?…Chonde mtoto chukua vyote kwangu ila kwenye rangi jitahidi uibe ya mama yako…..!!! nikavimbe Mtwara ?,” Harmonize aliandika kwa Instagram na kuweka picha ya mtoto wake akiwa tumboni mwa mpenzi wake.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere