Harmonize amtetea Zari vikali

Harmonize amemtetea Zari dhidi ya madai kuwa anaponda raha siku chache tu baada ya kumpoteza mama mzazi. Zari, Diamond na Harmonize walionekana Mombasa, Kenya wakijivinjari jambo ambalo halikuwapendeza baadhi ya watu.

Harmonize ata hivyo alimtetea Zari kwa kusema kuwa mtu akipata msiba alafu akapelekwa sehemu nzuri kwa ajili ya kufurahi ni kitu cha kumshukuru mwenyenzi Mungu. Alisisitiza kuwa maisha lazima yaendelee ata mtu akipoteza wapenzi wake.

download latest music    
Harmonize na Zari

“Kwa sababu haikuwa rahisi, unajua kufiwa na mazazi sio kitu kidogo. Tumefika (Mombasa) tumemkuta yupo fresh, yaani kasharidhika na matokeo kwa sababu anajua hakuna binadamu atakuja kuishi milele. Kwanza ukiona mtu anazungumza hiyo ujue haijui dini, kwa sababu dini imeandika kila mtu atakufa, kifo ni kitu cha lazima, ukiwa unaijua dini huwezi kuhofia suala la kifo. Mtu kafariki ni lazima uumie ila ni lazima maisha mengine yaendelee kwa sababu hata ukae ndani miaka sita hawezi kurudi,” Harmonize ameiambia kipindi cha XXL ya Clouds FM.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere