Harmonize Awaomba Radhi Mashabiki Wake.

Msanii wa muziki kutoka lebel kubwa  ya wasafi  Harmonize ,kwa takribani siku kadhaa nyuma amekuwa akiweka picha  za kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa kibao chake kipya kilichotakiwa kachiwa hewani siku ya tarehe 01 March mwaka huu,

Lakini kutokana na sababu ambazo Harmonize mwenyewe ameshindwa kuzisema , ameshindwa kutoa wimbo hu uliojulikana kama kwangaru ambao amemshirikisha boss wake Diamond Platinumz.

download latest music    

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram ,Harmonize amewaomba msamaha mashabiki wake kwa kuwasubirisha kwa muda mrefu na badoa meshindwa kutimiza ahadi yake ya kuachia wimbo huo.

Hata hivyo sio mashabiki wote wa msanii huyo wameweza kumuelewa msanii huyo huku wengine wakimtolea maneno  makali na kumwambia kuwa alikuwa akitengeneza kiki tu ili kuvuta attention ya watu.Mpaka Harmonize anaomba msamaha hajasema kuwa ni lini tena anatarajia kuutoa tena wimbo huo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.