Harmonize Awasihi Mashabiki Wasimchonganishe na Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘ Kwa ngwaru’ Harmonize ameibuka na kuwasihi mashabiki zake wasimchonganishe na msanii mwenzake Ali Kiba.

Kwa muda mrefu kumekuwa na sintofahamu kati ya Diamond na Ali Kiba hali iliyosababisha kuwepo hata kwa uadui kati ya wasanii wa WCB au watu wake wa karibu na watu wa karibu wa Ali Kiba.

download latest music    

Siku ya Jumapili kwenye viwanja vy Leaders Club Ali Kiba na Diamond walizua gumzo baada ya kusalimiana msibani kuonyesha kama hakuna tofauti baina yao.

Lakini Harmonize alikaaa pembeni ya Ali Kiba lakini kilichowashangaza watu wengi ni baada ya kuonekana hawajaongea neno hata moja yaani kiufupi walichuniana.

Baadae mashabiki walimjia juu Harmonize na kudai alimchunia Ali Kiba hakumpa hata salamu wakati bosi wake Diamond alijishusha na akamsalimia Ali Kiba.

Harmonize amemtolea povu shabiki kupitia mtandao wa Instagram na kumtaka asimgombanishe na Ali Kiba:

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.