Harmonize azungumzia kuhusu mjengo wake

Muimbaji kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka kuhusu mjengo wake ambao ni wa ghorofa akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni.

download latest music    

Kulingana na Harmonize mjengo wake unawezekano wa kukamilika mwishoni wa mwaka huu. Hata hivyo, Harmonize alikataa kufunguka kuhusu gharama aliyotumia kutengeneza ghorofa hiyo.

Harmonize alisema;

“Kwa hiyo flow ya kwanza tayari bado ya pili, kidogo kidogo tunajikongoja tukipata 200 tunaweka. Sio kitu kizuri kusema (gharama) nadhani lakini imetumia hela nyingi”

Harmonize aliendelea kwa kudai….

“Siwezi nikakadiria lakini imekula hela nyingi, show zenyewe hizi kwa mwaka sita/saba na usawa wenyewe ulivyo mgumu lakini nashukuru sio show pekee zinazonipatia hela kuna mishe nyingine, kwa hiyo siwezi kujua ni kiasi gani imekula lakini imekula hela nyingi,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua