Harmonize- Namuheshimu Wolper Ameona Utupu Wangu

Mwanamuziki kutoka WCB, Harmonize anayetamba na nyimbo zake mbili zinazofanya vizuri ‘shulala’ na ‘nishachoka’ amefunguka na kusema anamuheshimu sana Wolper kwa sababu ameona utupu wake.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na attention kubwa sana iliyoelekezwa kwa Harmonize na mpenzi wake wa zamani wake Jacqueline na mpenzi wake wa sasa Sarah. Sakata hilo lilianza tangu Wolper alipoachana na Harmonize na kuweka wazi kuwa Harmonize yupo na Sarah kwa sababu ya pesa. Siku chache zilizopita baada ya Harmonize kutoa ngoma yake ya Shulala wanawake hao waliingia kwenye ugomvi mkubwa mpaka kusemekana kuwa Harmonize amerudiana na Wolper kitu ambacho Harmonize alichokataa.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Lil’ommy  Harmonize alikataa kuwa wimbo wake wa ‘nishachoka’ amemuimbia Wolper:

Unajua msanii mzuri ni yule anayeimba nyimbo zinazogusa maisha ya watu na mapenzi ni kitu kinachogusa watu wengi kwaiyo ule wimbo mi nimeimba ili niwafurahishe mashabiki wangu lakini sio kweli kwamba nimemuimbia Wolper, kuhusu kumtumia model anayefanana na Wolper halikuwa wazo langu mi nimeimba nyimbo director ndo akachagua model wa kuwepo kwenye video kwaiyo mi sijui lolote itakuwa vizuri umuulize director”.

Harmonize aliendelea zaidi kufunguka kuhusu Wolper na mchango wake;

Kikubwa naomba nimshukuru Wolper kwa kuiposti ngoma yangu na kuisapoti kwani ametumia muda wake, bando lake, image yake kaweka kwenye kazi yako  kwa kweli sio kitu rahisi, mi namheshimu sana na namshukuru sana naomba mwenyezi Mungu amjaalie na ukizingatia vitu vyote vilivyokuwa vinatokea kwenye mitandao ya kijamii yeye ndo alikuwa anazungumza kwenye media kwa sababu mimi sio mtu muongeaji sana alafu mi huwa namheshimu sana mwanamke ambaye ameona utupu wangu siwezi nikakaa nikamzungumzia vitu alivyokuwa anafanya”.

Baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Harmonize amemuimbia Wolper ule wimbo, baadaye  akatoa video ya wimbo wake wa Nishachoka na kuonekana wazi kabisa model aliyetumika anafanana na Wolper.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.