Harmorapa Aachana na Menejiment Yake Mpya Tena.

Msanii wa muziki Harmorapa ambae amekuwa akitengeneza kiki kila siku amekutwa na janga lingine tena la kutemwa na menejimenti yake mpya ambayo amesaini nayo mkataba siku sio nyingi kwa makosa yale yale aliyokuwa ameyafanya mwanzao katikamenejiment yake ya zamani.

Harmorapa ambae miezi kadhaa huko nyuma ilisemekana kufulia kabisa kutokana na kuachwa na menejiment yake baada ya kufanya kazi nje ya menejiment kinyume na makubaliano ya mkataba na kushindwa kumpa meneja wake hata sent tano  alipata bahati ya kuwa na uongozi mpya lakini inasemekana kuwa hata hiyo wameshindwana nayo.

download latest music    

mpaka sasa hakuna aliyeweka wazi juu ya kuachana kwa meneja mpya na msanii Harmorapa lakini tetesi zinasema kuwa msanii huyo ameshindwa kufanya kazi na menejimenti hiyo kwa sababu harmorap aliamua kufanya kazi  nje ya menejiment hiyo bila taarifa wa uongozi wake kitu ambacho ni kinyume na makubaliano

Msanii huyo ambae amezoea kufanya kazi kwa kiki anaonekana kutokutulia na kuwafanya hata wasanii wenzake kumsema vibaya kuwa amekuja katika tasnia ya muziki kwa ajili ya kutafuta jina tu, na watu kama hawa hawakuzi muziki bali wanaua.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.