Harmorapa aeleza sababu za kutomiliki bastola kama wasanii wenzake

Image: Harmorapa

Ni kweli kuwa Harmorapa anatisha wasanii wenzake ambao amewaonyesha kivumbi muda mfupi baada ya kuwa staa maarufu Tanzania.

Sasa hivi anapesa zake na anamiliki gari kubwa lakini bado hajafikiria kumiliki bastola yake kwa kuwa ana ulinzi wa kutosha. Alizungimza katika kipindi cha Dj Show cha Radio One, Harmorapa alieleza kuwa bado hajafikiria kuwa na bastola kwakuwa ana personal bodyguard ambaya hutembea na yeye kila mahali aendapo.

download latest music    

“Sasa hivi nina pesa nyingi, nina gari nini. Lakini sijawaza au kufikiri siku nije kumiliki bastola kwa sababu eti nina pesa sijawaza kwa muda huu ila sijajua huko mbeleni iatkuwaje,”

Aliendelea kwa kusema kuwa ulinzi alionao hauwezi kubali mtu amkaribie. Kulingana na yeye bodyguard wake ameshiba tosha na ndio maana haoni haja ya bastola.

“Nikisema kwaajili ya kujilinda unajua sasa hivi mimi nina bodyguard wangu ameshiba na ameenda hewani. Hata ninapokaa kwenyewe nina ulinzi mpaka umfikie Harmorapa kuna kazi kubwa sana na unaweza usionane naye,” ameongeza.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua