Harmorapa afunguka kuhusu uhusiano wake na Amber Lulu

Rappa kutoka Tanzania Hamorapa hivi karibuni kudai kuwa yeye na Amber Lulu wanatoka kimapenzi. Msanii huyu alikiri haya baada ya wengi kudhania kuwa uhusiano wao ni wa kiki.

download latest music    

Hii inakuja baada ya Lulu Diva kukana kuwa anauhusiano na Harmorapa. Hata hivyo rappa huyu ameiambia Boys Boys ya TV1 kuwa yeye kama mwanaume lazime awekatika mahusiano. Harmorapa alisema;

“Unajua siku zote kama ni mwanaume, halafu mwanaume rijali ni lazima uwe kwenye mahusiano ya kimapenzi, kwa hiyo mimi nina mpenzi, kuoa bado hata mtoto sina. Kwa sasa ni mtu famous, nilishamtaja ili kuna wengine hawamfahamu ni Amber Lulu,”

Hata hivyo hatujui ikiwa ni kweli hawa wawili ni wapenzi.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua