Harmorapa amsifia Alikiba kwa kusema haya

Harmorapa ni msanii ambaye anaitambua kazi ya Alikiba na ingawa wawili hawa hawajapata nafasi ya kukutana…hii haimaniishi kuwa Harmorapa hatamani kufanya kazi na King Kiba.

Katika interview aliyoifanya hivi karibuni, Harmorapa alidai kuwa Alikiba ni msanii mwenye bidii na watanzania wanapaswa kuitilia kazi yake maanani kwa sababu Kiba anabusara kuwashinda wengi Wa kisasa. Harmorapa alisema,

download latest music    

Katika vitu ambavyo tunatakiwa kujivunia ni kuwa na wasanii ambao wanatangaza taifa letu mbele na kujivunia juhudi zao. Naimani heshima, busara na juhudi ndiyo nyenzo pekee wazungu kumwaga wino na kumkaribisha Alikiba meza moja na kumkabidhi kampuni kubwa ya Rockstar4000 kuwa mmiliki mmoja wapo na Director.

Rapa huyu wa Tanzania aliendelea kusisitiza kuwa wasanii wanafaa kujifunza na kujivunia uwepo wa Alikiba kwa kuwa muziki wa bongofleva ulitambulika zaidi baada ya Alikiba kuachia nyimbo zake za kwanza.

Wasanii wa Tanzania inabidi tujifunze na kujisifu kwa kuwa na King Alikiba maana anautendea haki mziki wetu wa bongo fleva, hongera zangu zizidi kutiririka kwa King wewe uliokosa mfano hapa bongo.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua