Harmorapa Atimulia na Meneja Wake Kufuatia Tuhuma Za Kumuibia

Msanii wa Bongo fleva Harmorapa ameingia matatani baada ya Meneja wake kumtimua chini ya uongozi wake baada ya kumtuhumu kumdhurumu pesa.

Harmorapa alitawala vichwa vya habari kwa mwaka huu wa 2017 hasa kwa sababu ya vituko vyake na kupenda kiki. Kuanzi bifu lake na harmorapa baada ya kutumia jina lake kupatia umaarufu mpaka kumganda na kumganda mrembo Wema Sepetu na kukiri mapenzi yake kwake.

download latest music    

Lakini kwa hIvi sasa Harmorapa anasemekana kupitia kipindi kigumu kwani aliyekuwa meneja wake mwanamama Irene Sebuka anasemekana kamtema. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mitandaoni ni kuwa Harmorapa alifuatwa na promoter mmoja na kuzunguka naye mikoani kwenye kufanya show mbali mbali lakini hawakua wakimletea manager wake mrejesho wowote wa mapato waliyopata kwenye show hizo alizokuwa anafanya.

Meneja wa Harmorapa alisema alisikitishwa na usaliti huo uliofanywa na aliyekuwa msanii wake ukitegemea kuwa aliytumia zaidi ya shilingi milioni 70 za kitanzania kumuibua na kumtangaza Harmorapa.

Irene amedai kuwa msanii huyo (Harmorapa) alirubuniwa na promoter huyo hivyo kumuona yeye meneja wake hana maana tena kwake hivyo ameamua kumtimua na kumrudisha kwa huyo huyo promoter aliye kuwa anamuona wa maana.

Harmorapa amekiri kosa na kuthibitisha habari hizo zina ukweli ndani yake lakini amedai kuwa yeye na meneja wake ni watu wanaojuana hivyo ana imani kuwa wanaweza wakakaa chini na kuyamaliza kama watu wazima na watasahemeana na kurudi kufanya kazi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.