Harmorapa Kafulia,Meneja Wake Aongea.

Harmorapa ni moja  ya wasanii waliokuja kwa kasi sana katika tasnia ya muziki huku wakiata kiki na kujulikana na mashabiki kwa muda mfupi sana,haha hivyo msanii huyo inasemekana kuwa amefulia na hana soko tena mjini, kitu ambacho mara ya kwanza msanii huyo alipoulizwa akikataa na kusema kuwa sio kweli kuwa amefulia ila kuna vitu bado anafatilia kwa sababu ana mambo mengi.

Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa harmorapa na meneja wake Irene Sebuka wamekuwa katika mgogoro uliomfanaya meneja huyo kumbaga msanii huyo na kuachana nae, hata hivyo chanzo hicho kinasema kuwa kwa kipindi fulani alitokea promota mmoja ambae alisema kuwa anamtaka msanii harmorapa ili wakafanye nae show mikoani lakini kitu cha ajabu ni kwamba walipoanza kufa nya show zao mikoani hakukuwa na mrejesho wowote  wa kumfaidisha meneja huyo kitu ambacho pia kilikwaza meneja huyo.

download latest music    

Akiendelea kumwaga ubuyu huo, alikuwa anatoa habari alisema kuwa promota na Harmorapa walikuwa wakienda mikoani kufanya show walikwa wakisemakuwa show hazikwenda vizuri ilhali meneja huyo akiangalia alishatumia zaidi yamilion 70 kwa ajili ya kumfanya harmorapa kujilikana mara alipokuja katika kiwanda cha muziki.

Akiongea na mwandishi kutoka Global meneja wa Harmorapa anasema kuwa anachojua yeye harmorapa alirubuniwa na promota bila kujali maslahi yake hiyvyo na yeye akaona isiwe tabu akaona bora kuachana nae.

Ninachojua huyo promota alitaka kumsaidia,kumbe alishajua Harmorapa amepata jina kwaiyo alitaka kumtumia.alitaka kumrubuni kwaio na mimi nikamuacha tu kwa sababu najua wapi nilipomtoa.  Aliongea meneja wa Harmorapa.

Hata hivyo Harmorapa alipotafutwa kuulizwa kuhusu jambo ilo alisema kuwa ni kweli amekuwa na matatizo ya hapo na hapo  na meneja wake lakini haimaaishi kuwa hawafanyi kazi pamoja.

kuna vitu vimetokea kweli lakini ninachojua ni kuwa mimi na irene bado tunafanya kazi, Irene bado ni meneja wangu. Amefunguka Harmorapa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.