Harmorapa Kumuendea Wema Sepetu Kwa Mganga Mara Tatu

Msanii ambae alijitambulisha katika tasnia ya bongo fleva kwa kiki nyingi sana lakini sasa kwa maneno ya chini chini ni kwamba msanii huyo amefulia na inawezekana kabisa akarudi kijijini kwao kutokana na kutemwa na menejementi yake, Harmorapa amefunguka na kusema ukweli kuwa kwa muda amekuwa akimtamani Wema Sepetu na mpaka ameshafikia hatua ya kumuendea kwa waganga wa kienyeji ili aweze kumpata lakini imeshindikana kabisa.

Harmorapa amesema kuwa amekuwa akiangaika sana kwa rafiki zake na Wema ili kumpata Wema lakini ilishindikana hivyo aliamua kwenda kwa sangoma na  kumfanyia dawa msanii huyo lakini cha ajabu ni kwamba mganga alimuagiza kuku mweupe  na akaleta lakini aliporudi mjini kuangalia mafanikio alikuta bado mambo si shwari kabisa.

download latest music    

Nilimuendea Wema kwa mganga mara ya kwanza mganga akaniambia nipeleke kuku mweupe nikapeleka lakini niliporudi Dar mambo hayakuwa sawa kwaiyo nikamuendea tena mabpo aliniagiza nipeleke vitu vingine tofauti mara mbili ambavyo hapa siwezi kuvitaja lakini naona b.ado

Harmorapa anasema kuwa amekuwa akipata wakati mgumu sana kuonana na msichana huyo kwa sababu kuna kipindi ameshaambiwa apeleke  hadi mchanga wa unyayo wa Wema Sepetu na mchanga wa alipotemea mate lakini imekuwa ikishindikana kwa sababu hapati nafasi ya kuwa karibu na Wema Sepetu.

Hata hivyo Harmorapa anasema kuwa kwa sasa ameamua kumuachia mungu swala la mahusiano yake na wema sepetu kwa sababu huko alikojaribu alishaangaika na ameshashindwa, kama bahati yake ipo basi atampta msichana huyo.Harmorapa ameshawahi kusema si zaidi ya mara  kuwa amekuwa akimtaka kimapenzi mwanadada Wema Sepetu .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.