Harmorapa Kurudi Kijijini Kwao

Mwaka 2017 ulikuwa ni mwaka wake, baada ya kuja mjini na kutafuta kiki ambayo aliipata bila gharama yoyote kutokana na drama nyingi alizokuwa nazo na kumfanya kujulikana karibia kila sehemu alipokuwa anakwenda watu waweze kumnyooshea vidole.

Msanii wa muziki aliyekuja kwa kazi huku baadhi ya wasanii wakimpiga vita sana kutokana na gia yake aliyokuwa ameingilia , Harmorapa  inasemekana kuwa maisha ya mjini yamemshinda na muda wowote atarudi kwao maeneo ya kusini baada ya kutimuliwa na meneja wake kwa kuwa mbabaishaji mjini.

download latest music    

Mara ya mwisho meneja wake aliyejulikana kama Irene Sebuke alisema kuwa walichoshindwana na Harmorapa ni baada ya kurubuniwa na moja ya mapromoter mjini kwa kumpa show za kumzungusha mikioani lakini kitu cha kushangaza meneja huyo akupata hata kiasi kidogo kutoka katika show hizo huku wakimdanganya kuwa walikuwa hawapati show ilhali ni uongo.

Hata hivyo meneja huyo alisema kuwa hrmorapa laiporubuniwa alionekana kumdharau kabisa meneja wake na kumjali sana promoter na kusahau kuwa nani alimleta mjini, hata hivyo harmorapa amekuwa akifichaficha tetesi hizo na kusma kuwa mambo yake na menehja wake yataisha tu huku akionekana mwenye hali mbaya.

Baadhi ya watu wa karibi na Harmorapa wanasema kuwa kwa sasa msanii huyo yuko mbioni kurudi kwao baada ya kuona kuwa meneja wake alishamkacha na maisha ya mjini yameshakuwa sio mazuri kwa uoande wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.