Harusi Ya Mchekeshaji Joti Imeiva

Msanii wa maigizo na mchekeshaji maarufu tanzania Joti, anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu hivi karibuni.msanii huyo ambae amekuwa akionekana katika matangazo ya bidhaa tofuati tofauti tanzania ameonekana  hivi karibuni katika mitandao ya kijamii yeye na mpenzi wake huyo katika picha za pamoja ikiwa ni pre-wedding photshop.

Joti ambae alianza maigizo ya uchekeshaji miaka mingi nyuma na baadae kuingia katika kundi la ze comedy waliokuwa wakirusha matangazo yao katika Televisheni ya Taifa anategemea kufunga ndoa na sherehe kufanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salam.

download latest music    

Akiandika katika moja ya post zake katika ukurasa wake wa instahram Joti aLiweka picha aliokuwa pamoja na mkewe huyo na kuandika “alilopanga mungu..” hata hivyo baadhi ya picha zilimuonyesha msanii huyo akiwa na rafiki zake wa karibu katika send-off party ya mke wake.

Baadhi ya mashabiki wameonekana kufurahishwa na jambo hilo na kumpongeza msanii huyo, huku wengine wakidhania ni utani kama ilivyozoeleka hapa awali ambapo Joti amekuwa akiweka picha za harusi na wadada tofauti  kumbe alikuwa katika moja ya kazi zake za matangazo.

Baadhi ya wasanii wenzie walimpongeza msanii huyo na mmoja wapo alikuwa ni mchekeshaji mwenzie  Masanja Mkandamizaji aliyempongeza kwa kuacha chama la makapela.

Moja ya picha zilizopo mtandaoni zikimuonesha joti akiwa na Sekion David katika send-off part ya mkewe

Joti akiwa na mkewe mtarajiwa katika picha ya pamoja katika send off party ya mkewe.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.