Hatimaye Mzee Majuto Kulipwa Mamilioni Yake

Muigizaji Mkongwe wa Bongo movie Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto anatarajiwa kuanza kulipwa mamilioni yake ya pesa aliyokuwa anadai katika mikataba mbali mbali.

Habari hiyo njema imekuja Miezi michache tangu Waziri Mwakyembe alipoyataka makampuni mbali mbali yaliyoingia mikataba na Mzee Majuto kisha kumlipa pesa ndogo au kumzulumu Kupitia mikataba hiyo na kumlipa Tena pesa zake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani Jumatatu iliyopita, nyumbani kwake, maeneo ya Bunju jijini Dar, Majuto alisema aliamua kusamehe ile mikataba midogomidogo ila kwenye ile mikataba mikubwa aliyodhulumiwa.

Niliamua kusamehe ile mikataba yangu midogomidogo ila hiyo mingine aliyosema ataishughulikia muheshimiwa Mwakyembe bado naendelea kuisubiri ila kwa sasa siwezi nikaongea chochote kuhusu hilo, hivyo naomba mumuulize msemaji wa chama cha waigizaji”.

Lakini pia gazeti hilo pia lilifanikiwa kuongea na msemaji wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni, Masoud Kaftany ambaye alisema hatua aliyofikia Mwakyembe ya ufuatiliaji wa mikataba ya wasanii akiwemo mzee Majuto inaendelea vizuri na hivi karibuni kila kitu kitakuwa sawa.

Siku ya jana Mzee Majuto alitangaza kuachana na mambo ya sanaa kutokana na maradhi mbali mbali yanayomsumbua.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.