Hatimaye Nawal Kafuta tatoo Ya Nuh Mziwanda

Wasanii wengi wa bongo wamekuwa na desturi ya kuchora tatoo  kubwa za wapenzi wao katika miili yao  wanapokuwa katika mahaba lakini shida huwa inakuja pale wawili hao  wanapoachana , ndipo yule aliechora anapoanza kuangaika jinsi ya kuitoka michoro hiyo katika miili yao.

Nawal ambae alikuwa mwanamke wa ndoa wa msanii Nuh Mziwanda aliamua kuchora tatoo ya mpenzi wake huyo ikiwa ni kama ishara ya mapenzi kwa mwanaume  wake lakin baadae wawili hao walikuja kuachana ivyo deni linabaki kwa mwanadada Nawal jinsi gani anaweza kuondoa alama ile kubwa katika mwili wake.

download latest music    

Wengi walikuwa wakisubiri ili kuona itakuwaje kwa mwanadada huyo lakini hatimaye amefanikwa na kuamua kufuta tattoo iyo lakina ameibadilisha na kuiweka  katika mchoro mwingine usioeleweka zaidi.Mwanadada huyo alisema kuwa ipo siku mashabiki wataamka tu na kuona tatoo iyo imeondoka na kweli amekamilisha maneno yako.

Muonekana wa tatoo mkononi mwa Nawal

Nuh  Mziwanda na Nawal walianza mahusiano na mahusiano hayo yali-trend sana katika mitandao kwa sababu ilikuwa ndicho kipindi ambacho Nuh Mziwanda alikuwa ametoka katika penzi la manyanyaso la msanii wa kike SDhiloleh ambae anasifika kwa kutembea na vijana chini ya umri wake.Nawal na Nuh walifanikiwa kufunga ndoa ya kiislamu baada ya mwanadada huyo kupata ujauzito.

Walifanikiwa kupata mtoto mmoja lakini baadae waliachana na mtoto kubaki kwa mama kutokana na umri mdogo alionao mtoto.Wawili hao waliingia katika ugomvi mkubwa baadae kuhusu malezi ya mtoto wao.

Nuh mziwanda amekuwa kila siku akilalamika katika mitandao Ya kijamii kutokana na malezi anayopewa mtoto huyo na mamake kwa madai kuwa mama yake na mtoto ambae ni Nawal amekuwa akienda kwa mabwana wengine au kuonekana kuwa bar akiwa na mtoto huyo mida mibaya ambayo mtoto hapaswi kuwa katika maeneo hayo.

Hata hivyo kuna kipindi baada ya mwanadada huyo kuachana na Nuh Mziwanda alikiri kuwa ameshaolewa na mwanaume mwingine na amekubali kulea mtoto huyo wa Nuh Mziwanda.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.