Hatma Ya Kesi Ya Hamisa dhidi Ya Diamond Kujulikana Leo

Miezi miwili iliyopita mwanamuziki Diamond Platnumz alikiri kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto, lakini baada ya wiki kadhaa Hamisa aliibuka na kudai kuwa Diamond amekataa kumuhudumia mtoto wao na kuwa alikuwa hatoi pes yoyote ya matunzo hali iliyopelekea kumfungulia kesi ya madai katika mahakama ya Kisutu’

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu siku ya leo Novemba 10, 2017 inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya kesi ya matunzo ya mtoto, uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu mkazi Devota Kisoka upande wa watoto.

download latest music    

Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kusikiliza hoja za pande zote husika kutokana namsaini Diamond kuwasilisha pingamizi kupinga kesi hiyo kwa madai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.

Katika kesi hiyo Hamisa alifungua kupitia kwa mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Goodluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys ambapo anaiomba mahakama imuamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi kupitia hati hiyo ya madai, mwanamitindo huyo anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoshtua familia yake.

Hata hivyo Diamond aliwasilisha hati ya majibu ya kinzani akipinga maombi hayo akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ni sh. milioni tano kwa ajili matunzo ya mtoto ni kubwa sana na hawezi kuzimudu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.