Hawa Ndio Wanawake Waliomtesa Diamond Kwenye Mapenzi.

Diamond ni moja wa wasanii wanaosemekana kuimba nyimbo nzuri na kupendwa na mashabiki kutokana na kuimba nyimbo zinazotoa historia ya maisha yake kila siku.Hivi juzi Diamond alitoa audio mbili mfululizo ya Sikomi na Niache, nyimbo ambazo zimepokelewa vizuri sana na mashabiki kwa sababu zimeelezea kwa undani kabisa maisha yake ya mapenzi na kuwataja wanawake wake wote ambao aliwahi kuwa nao katika mahusiano na vitendo vya kikatili walivyomfanyia katika mapenzi.

Hawa ndio wanawake haliowataja diamond katika nyimbo zake hizo.

download latest music    

WEMA SEPETU.

Aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2016, baadae alikuja na kujiingiza katika tasnia ya bongo movies.Ni moja kati ya wasanii wa kike maarufu na wanaopendwa na kuongoza katika mitandao kuwa na mashabiki wengi sana.Alishawahi kuwa na mahusiano na watu wengi maarufu na kila siku amekuwa ni mwanadada mwenye drama nyingi sana katika mapenzi.Alishatoka na Mr. Blue, Idris Sultan, na Steven Kanumba.

Ukiachana na urembo lakini pia Wema anajihusisha na ujasiriamali wa vipodozi.Amekuwa ni moja ya wanadada wanaojisifu kuwa na application inayoelezea maisha yake inayopatikana Playstore.

VJ PENNY

Kwa sasa ni mtangazaji wa kipindi kimoja cha harusi katika television moja nchini, jina lake lilipata umaarufu sana alipokuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond, huyu ndie diamond aliemlilia baada ya kupata mimba na kuitoa ilhali diamond alikuwa akitamanai mtoto

HAMISA MOBETO

Ni mwanamitindo ambae kwa sasa amaeona fursa nyingine kupitia uigizaji, alikuwa na mahusiano na Diamond kwa muda mrefu lakini yalikuwa ni siri yao, alikuja akapata mimba na Diamond aliikataa ktika mitandao na vyombo vya habari.Baada ya kutoa ushaidi wa mahusiano yao Diamond alikubali  majukumu ya mtoto wa mrembo huyo.Ameingia katika vichwa vya habari kutokana na mahusiano yake na Diamond kwenda mrama mpaka kufikia hatua ya kupelekana polisi.Amezaa na Diamond mtoto mmoja.

ZARINA HASSAN

Ni mama wa watoto watano lakini wawili kazaa na Diamond, ni mwanamke inaesemekana kuwa amesaidia kwa kiasi kikubwa sana mafanikio ya msanii huo.ni mwanamama kutoka Uganda, mwenye utajiri mkubwa alioachiwa na baba mzazi wa watoto wake watatu wa kwanza.aAmepitia misukosuko mingi ya kimahusiano  na msanii Diamond lakini  bado wapo pamoja.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.