Hemed PHD ni Chawa Wangu- Gelly Wa Ryhmes

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gelly wa Rhymes amefunguka na kudai kuwa msanii mwenzake wa Bongo fleva Hemed PHD pia ni chawa wake.

Hemed na Belly wamekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 11 wameshirikiana na kudhirikishana katika nyimbo zao mbali mbali lakini wameigiza pamoja filamu za bongo movie kadhaa na kwa nyakati tofauti wote wamesisisitiza kuwa wao kwa sasa ni zaidi ya marafiki wamekuwa kama ndugu kwa ukaribu wao.

download latest music    

Gelly amejibu fununu zilizopo mtandaoni zinazodai kuwa yeye ni chawa tu wa Hemed na hana mchongo mwingine wa maana hapa mjini, Gelly amesema yeye na Hemed ni zaidi ya ndugu hivyo watu wanaomuita chawa wake hawafahamu kuwa hata Hemed ni chawa kwake.

Gelly alifunguka hayo kwenye mahojiano na Enews ya EATV ambapo pia alizidi kuongeza:

Kwanza nilikuwa sielewi maana ya chawa mpaka uliponielezea kumbe chawa ni mtu ambaye yuko karibu na mtu basi kama ndio hivyo Hemed basi na yeye chawa wangu kwa sababu na yeye yupo karibu na mimi sana, anyway iko hivi mimi na Hemed sahivi tumevuka urafiki tuko kama brothers na ni watu tunaosaidiana kwenye kila kitu hata kutoa nyimbo lazima tushauriane kwaiyo tuko pamoja most of the time hasa hasa kikazi hata yeye akiwa na tatizo ananifuata ananiambia na mimi pia nafanya hivyo hivyo”.

Lakini pia Gelly ameongelea label yao pamoja naHemed inayoitwa Pappination lakini pia nyimbo yake aliyoitoa hivi karibuni inayoitwa ‘Vibenten’ ambayo ndani yake ameongelea vijana wa mjini ambao nivibenten lakini pia amedai amewataja kwa majina humo ndani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.