Hemedy PHD: Mimba ya Mapacha ya Girlfriend Wangu Imetoka ghafla, Lakini Ningekuwa na Watoto 8

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamuziki wa Bongo fleva, Hemed PHD amefunguka kuhusu tuhuma anazorushiwa kwa kitendo kinachosemekana kuwa amewaacha solemba watoto wake watano na kumuweka wazi mmoja tu.

Hemedy ni moja kati ya wasanii anayesemekana kuwa na watoto wengi ambapo amesema kuwa ana watoto sita. Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni Hemed amekiri kuwa na watoto wengi kiasi kuwa wengine ni ngumu kuwatambua kwani kipindi cha nyuma alikuwa anakataa mimba nyingi.

download latest music    

Pamoja na kuwa na watoto wengi, kupitia ukurasa wake wa Instagram na mitandao mingine yote ya kijamii Hemed humweka wazi mtoto wake mmoja tu na hivyo kupelekea watu wengi kudhani kuwa ana mtoto mmoja tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa radio, Hemed alifunguka haya kuhusiana na tuhuma hizo na tetesi za kuwa na watoto sita:

Kwanza naomba niseme kuwa namshukuru Mungu kwa kila kitu kilichotokea kwenye maisha yangu kwa sababu wiki mbili zilizopita mpenzi wangu alipata miscarriage na ilikuwa mimba ya mapacha kwahivyo ningekuwa na watoto nane na mtoto wangu wa kwanza ana miaka mitatu na wanaofuatia wote watano wamepishana miezi miwili miwili na kila mtoto na mama yake”.

Pia Hemed alifunguka kuhusu tuhuma za kuwatenga watoto wake wengine na kumuonyesha mtoto mmoja tu ambapo amedai kuwa mama za watoto wake wengine hawapendi awaanike watoto wao kwenye mitandao ya kijamii hivyo anaheshimu maamuzi yao na kuwaweka private na pia kuna ugomvi wa kifamilia baina yangu na wamama hao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.