Hii Ndio Sababu Iliyomzuia Wema Kufika Kwenye Uzinduzi Wa Filamu Ya Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kutaja sababu iliyomfanya mpaka asiweze kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Aunty Ezekiel.

Siku ya Jumapili Aunty Ezekiel alikuwa anafanya uzinduzi wa filamu yake fupi ya dakika 20 inayoitwa MAMA pale Kwenye ukumbi wa Cinema Mlimani City.

download latest music    

Wema Sepetu ambaye mwanzoni alitoa taarifa ya kuthibitisha kuwa atakuwepo eneo la tukio kumpa sapoti Aunty Ezekiel ambaye pia ni rafiki yake kipenzi kabisa hakuonekana mpaka shughuli inaisha.

Siku ya jana Wema aliweka wazi kuwa sababu kubwa iliyomfanya mpaka asihudhurie shughuli hiyo ilikuwa ni kucheleweshwa na Mama yake mzazi ambaye alikuwa naye na hivyo kujikuta kapitisha muda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema aliandika:

I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa…???,”

Hata hivyo Aunt Ezekiel alipohojiwa na Mwananchi Digital sababu za Wema Sepetu kushindwa kufika katika uzinduzi huo alisema ni kutokana na gauni la mrembo huyo alilotakiwa kuvaa kwenye uzinduzi huo lilikuwa bado lipo kwa fundi halijamalizika kwa sababu ya kukatika kwa umeme.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.