Hii ndiyo sababu ya Chid Benz kumchana Chin Bees

Chid Benz ambaye ni mmoja wa wasanii wa hip hop walioanza kuachia nyimbo zao kitambo ameonelea kumkanya Chin Bees ambaye anatumia jina linalokaribiana na staa huyu.

Sababu za Chidi Benz kumwambia Chin Bees atafute jina lingine ni kwa sababu majina hayo yanafanana na kunauwezekano wa kuwakanganya mashabiki wake.

download latest music    

Ingawa wawili hawa wanafanya nyimbo tofauti Chid Benz anamtaka Chin kuwa mbunifu na kutafuta jina ambalo halifanani na lake. Msanii huyo alisema,

“Siku moja nimeona Shetta anamuangalia Instagram nikamuuliza huyo ni nini?, akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani, akaniambia Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya yeye ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia kwenye stage nachapa tu,”

Akipiga stori na Planet Bongo ya EA Radio aliendelea kusema;

“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina lingine,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua