Hii ndiyo sababu ya Diamond kukosa kuhudhuria matanga ya Ivan licha ya kudhibitisha awali kuwa angehudhuria

Akiongea kwenye kipindi ya The Trend ya NTV Kenya Ijumaa iliyopita, Diamond Platnumz alisema kuwa atasafiri kuenda Uganda kuhudhuria matanga ya Ivan Ssemwanga baada ya kumaliza show yake Nairobi.

“Well kwa ukweli ulikua ni wakati mgumu na mbaka saa hivi ni wakati mgumu kwasababu nlikua nko booked muda kidogo kuhusiana na Korogo festival, na msiba umetokea sasa kucancel tu ghafla show ya watu unajua inawezekana ukapata taswira tofauti, wengine wakachukua tofauti. Sikua na jinsi. So, lakini nliongea na mzazi mwenzangu (Zari) akanielewa, lakini nikimaliza hapa show tu na ntaenda Uganda kwasababu ya mazishi, kuzika. Baada ya hapo ndo ntarudi nyumbani,” Diamond alisema.

download latest music    

Lakini hata hivyo jana Simba hakuonekana kwa matanga ya Ivan, kwasababu gani? Meneja wa Diamond Sallam Sharaff alisema kuwa msanii huyo hangeweza kusafiri kwenda kumzika Ivan kutokana na ratiba kuingiliana.

“Kwenye mazishi hatujahudhuria, ilikuwa twende leo alfajiri lakini sasa kumbe wao wametoka usiku kwenda kijijini. Kwa hiyo nadhani ratiba yetu imeingiliana maana na sisi tulitoka Nairobi jana jioni.” Sallam alikiambia kipindi cha U-heard cha Clouds FM.

Skiza Sallam akielezea kwanini Diamond hakuweza kusafiri kuenda kumzika Ivan hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=elxy8DgyaFo

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere