Hii ndo sababu Mheshimiwa Goodluck Mlinga anataka serikali kujenge sanamu ya Diamond

Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga amesisitiza kuwa ni lazima serikali iwatambue wasanii wanaowakilisha Tanzania vizuri nje.

Mheshimiwa huyo alisema bungeni kuwa Diamond anastahili kujengewa sanamu kwasababu anawakilisha nchi vizuri kimataifa. Mlinga alipendekeza kuwa sanamu la askari posta Dar es Salaam liondolewe na kuweka hilo la Diamond.

download latest music    

Akiongea na Habari Xtra ya Times FM, Mlinga alieleza kuwa Diamond ni mmoja tu ya wasanii ambaye yeye anawapigania ili serikali iwatambue kwa kazi zao nzuri.

Mheshimiwa Goodluck Mlinga alisema

 

“Na sikumtaja Diamond pekee, niliwataja wasanii wengi kama wakina Mr Nice ambao wameiwakilisha Tanzania sana nje lakini mpaka leo hii wamepotea hawana alama, inakuwa hawawezi kuwahamasisha wasanii wengine, lakini tunapoweka alama kila msanii anapofanya vizuri tunahamasisha wengine na ndiyo utaratibu katika nchi za wenzetu. Kuna mchezaji mmoja wa mpira alitoka Kenya (Victor Wanyama) kuja Tanzania siku ya pili alipewa mtaa, sasa vile vitu ndio tunatakiwa tuvifanye kwa wasanii wetu wanaoibeba nchi. Sasa wewe fikiri mtu katoka nje ambaye anawakilisha nchi nyingine tunampa mtaa, lakini kwetu ni msanii gani alishawahi kuacha alama hata akapewa Barabara, hakuna!!!,” Mheshimiwa Goodluck Mlinga alisema.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere