Hisia za Gabo Kuhusu Hukumu Ya Lulu Michael

Ni watu wengi wameonekana kuumizwa na hukumu ya msanii Lulu Michael baada ya kuhukumiwa miaka miwili gerezani. Watu wengi wwameonyesha hisia zao katika hilo tena wengi wakiwa wanaonekana kuumia kwa kitendo hicho, wengine walikuwa wakimuombea ili aachiwe na asikutwe na kifungo lakini leo Novemba 13 mahakama imemkuta Lulu na hatia ya kuua bila kukusudia na kumtumikisha kifungo cha miaka miwili jela.

Lulu ambae alikuwa ndio ameanz akufanya vizuri na kuwakilisha vyema katika tasnia ya filamu leo hii anafanya watu wakate tamaa na kuona kama pia tasnia inakoelea ni kubaya zaidi.

download latest music    

Akiwa kama mmoja wa watu wa karibu hasa katika swala la kazi msanii wa filamu nchi Gabo Zigamba  ameonyeshwa kusikitika lakini pia imekuwa kama akiitolea lamawa mahakama kwa kesi hiyo na hukumu yake kumuhusu Elizabeth Lulu Michael.Katika ukurasa wake wa instagram msanii Gabo alisema kuwa mahakama pia ilitakiwa kwa upande mwingine iangalie mahusiano aliokuwa nayo marehemu na mtuhumiwa ambae kipindi hicho alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi angali na umri mdogo.

Wacha niridhike na sauti ya kunyamaza huku mtima wangu ukiwa na majonzi na maswali tele,…hivi Kanumba angekuwa hai asingeshitakiwa kwa kuishi kinyumba na mtoto wa chini ya miaka 18,miaka? #anzakanuni#RIP-  Aliandika Gabo

Mama wa kanumba alionesha shukrani yake kwa mahakama kwa kutenda haki juu ya hukumu iyo huku mama wa msanii Elizabeth Lulu Michael  akilia mpaka kushindwa kutemba kutoka katika mahakama hiyo.hii itakuwa ni moja ya marudio ya kilio cha mama mzazi wa msanii huyo ambae kipindi kesi inaanza miaka kama mitano iliyopita alikuwa akionekana mwenye majonzi kutokana na kile kilichokuwa kikimkabili mtoto wake.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolewa wakili msomi wa Lulu Michael, Peter Kibatala alisema kuwa hakuridhishwa na hukumu ya mahakama kwa mteja wake hivyo anategemea kukata rufaa hili kumpunguzia  adhabu ya hukumu hiyo msanii huyo.Hivyo endapo rufaa itakubalika kesi hiyo itaweza kusikilizwa na msanii huyo kupunguziwa adhabu iliyotolewa leo ya kukaa gerezani miaka miwili.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.