Hizi Ndo Sababu Watu Wanadai Kuwa Wolper Kaachana na Mpenzi Wake

Muuigizaji wa Bongo Movie na mrembo Jacqueline Wolper anadaiwa kuachana na Mpenzi wake Brown.

Habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinasema kuwa Wolper na mpenzi wake wameachana kwa muda mfupi sasa.Huku hakuna hata mmoja kati yao aliyekataa au kuthibitisha habari hizo mpaka hivi sasa lakini kuna tetesi zinazoenea chini ya kapeti zinadai hivo.

download latest music    

Wolper kafuta picha zote za Brown kwenye ukurasa wake wa Instagram na Brown naye kafanya hivyo hivyo pia. Katika mapenzi yao wawili hao walikuwa watu wakupiga picha pamoja na kila mmoja kuziposti kwenye kurasa zao sasa ilipotokea siku mbili hizi kila mmoja kafuta picha za mwenzake ndipo watu walipoanza kuhidi kutakuwa kuhlna jambo linaendelea baina yao.

Pia sababu nyingine inayopekekea watu kuhisi wawili hao wameachana ni kitendo cha Wolper kuenda kwenye sherehe ya birthday ya Diamond ambapo alijua kabisa atakutana na mpenzi wake wazamani Harmonize na pia Wolper alienda kwenye sherehe hiyo mwenyewe bila Brown ambaye ni mpenzi wake na pia habari za udaku zinasema Wolper alionekana akipeana mkono na Harmonize.

Inasemekana kuwa Brown alikuwa amechora tattoo ya Wolper kifuani lakini kwa picha inayosambaa mtandaoni inaonyesha wazi kuwa amekwishaifuta tatoo hiyo ikimaanisha wameachana.

Je kutokana na sababu hizo unahisi kuna ukweli wowote wa Wolper na Brown kuachana?

Toa maoni yako tafadhali.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.