Hoja ya Mange kimambi Aibuka Tena Bungeni.

Mwanadada mange kimambi  mwanaharakati maaarufu anaekaa nchini Marekani lakini amekuwa akitetea na kuibua mamno mengi katika jamii hasa ya Tanzania, ameibuka tena kama hoja bungeni baada ya mbunge wa Ulanga Mh Mlinga kuitaka serikali kupitia mamlka ayake husika kushughulika na watu wote hasa katika mitandao ya kijamii wanaotukana viongozi wa nchi.

Mh Mlinga anasema kuwa kutoka na kuwepo kwa kurasa nyinngi zenye kufanya mambo hayo kumekuwa hakuna tena heshima wala cheo cha rais au viongozi wake kwa sababu viongozi wamekuwa wakitukwanwa bila kuogopa kitu.

download latest music    

matusi katika mitandao ya kijamii ni too much, haijulikani katika mitandao rais ni nani  au kiongozi ni nani, kumekuwa na akaunti nyingi zinatukana sana katika mitandao ya kijamii , IGP huko hapa tumekuwekea hizo nyota mabegani  ni nguvu, tumia nguvu zako ,mfano natoa akaunti zinazomtukana raisi ni pamoja na Kwinyara, Malisa gj, Yerico Nyerere na dada yao Mange Kimambi wamekuwa wakimtukana sana rais.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa viongozi kutaka mwanadada huyo kuchukuliwa hatua kwa tuhuma hizo ingawa kunamengipia mazuri ambayo mwanadada huyo amekuwa akiyafanya katika jamii, lakini yote yanaweza kutambulika kulinagana  na mamlaka husika.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.