Huddah Awachana Wabongo Kwa Unafiki Amkingia Kifua Jokate

Socialite maarufu kutoka pande za +254 Kenya, Huddah Monroe amewatolea uvivu wabongo kwa vitendo vya kinafki walivyomfanyia Jokate Mwegelo mara baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya.

Huddah amewatolea povu watu waliomnanga Jokate baada ya Ali Kiba kumuoa mwanamke mwingine ambaye ni Amina mwaka huu na kusababisha watu kumcheka sana Jokate.

download latest music    

Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Snapchat Huddah ameandika ujumbe huu:

Ali Kiba alivyomuoa msichana mwingine mapema mwaka huu watu walimcheka sana na kumdhalilisha Jokate. Lakini sasa hivi anapata mafanikio hao hao watu wanageuka na kumpongeza ama kweli mitandao imeshindikana. Hana mashabiki wa kweli bali ni wanafiki tu na wanaondoka kwa upepo”.

Ali Kiba alikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Jokate kwa muda mrefu lakini mapema mwaka huu alimuoa Amina.

Wikiendi iliyopita Rais Magufuli alimtangaza Jokate kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe jambo lilipelekea kupata pongezi nyingi sana kutoka kwa mashabiki mbali mbali na hata wasanii wenzake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.