Huu ndio ujumbe ambao Shamsa Ford aliwapa wanaume hawapendi kufanya kazi!

Staa wa muvi za Bongo Shamsa Ford hivi karibuni alichukua muda wake kuwa shauri wanaume amabao hawapendi kujitegemea – haswaa wale ambao huchagua kazi za kufanya.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Shamsa alionekana kukerwa na wanaume ambao wanategemea kufugwa na wanawake wazee kuwashinda.

download latest music    
Shamsa Ford

Katika ujumbe wake msanii huyu alitaja kuwan I vizuri wanaume kujituma na kufanya kazi kwa mikono yao badala ya kutamani maisha ya haraka yasiyo na utamu wowote. Aliandika kusema;

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,”

Akaongeza;

“Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua