Huyu Ndio Mume Mtarajiwa Wa Jacqueline Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper hatimaye alitangaza kuwa ana mpango wa kuolewa wiki iliyopita na hatimaye mume mtarajiwa amejulikana.

Jacqueline aliwashtua watu wengi baada ya kutangaza kuwa ana mpango wa kuolewa ikiwa kiukweli ulikuwa hata gaujapita hata mwezi tangu ameachana na mpenzi wake aliyekuwa naye kwa miezi michache Brown au BFF.

download latest music    

Ingawa aliweka wazi kuwa anaenda kutolewa mahali kwao Moshi lakini pia aliweka wazi kuwa hana mpango wa kumuweka wazi bwana harusi kwa kile alichodai kuwa anaogopa kuibiwa lakini mapaparazi wa mjini wamemtafuta na hatimaye sura yake imeonekana.

Jamaaa huyo aliyemchumbia Wolper kijijini kwao Moshi kwa Bibi yake na inasemekana kuwa kwa jina anaitwa Sadick Athanas lakini jina lake la umaarufu anaitwa Engine na pia ni msanii chipukizi wa mziki wa Bongo fleva.

Gazeti la Amani limeripoti kuwa sherehe ya kuchumbiwa kwa Wolper iliyofanyika wikiendi iliyopita ilizua gumzo la aina yake baada ya muoaji kufanya kufuru ya aina yake inasemekana sherehe hiyo ilihusisha msafara Mkubwa wa magari kutoka Dar es Salaam kuelekea Moshi kijijini.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.