Huyu ndiye msanii wa Kenya ambaye Harmorapa anataka collabo naye

Harmorapa anamipango ya kutamba nchini Kenya na kwa sababu hii amemtaja msanii ambaye amekuwa akitaka kufanya kazi naye kwa muda sasa.

Akizungumza na Bongo 5 msanii huyu ambaye anafanya vyema nchini Tanzania alisema kuwa anamkubali Prezzo na anaipenda kazi yake. Aliweza kueleza kwa sasa msanii ambaye angependa kufanya at least project moja na yeye nchi za Afrika Mashariki ni Prezzo peke yake.

download latest music    
Prezzo
Prezzo

“Prezzo namkubali sana toka kitambo, tokea niko chini shule ya msingi. Nilikuwa namkubali sana swagga zake na rap zake zilikuwa zinanifurahisha sana na zinanifurahisha mpaka kesho kiukweli.”

Aliendelea kusema iwapo atapata nafasi, Afrika mashariki itaweza kuona collabo yake na Prezzo. Lakini kwa sasa anangoja nafasi hii ikitokeze na kwa kiukweli ataweza kuifanya Tanzania proud.

“So kwahiyo natamani sana one day nifanye naye collabo kwahiyo kama nikipata nafasi kufanya naye itakuwa very good nitashukuru Mungu,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua