Idris Ataja Wanawake Anaowaogopa Duniani.

Msanii na mchekeshaji maarufu bongo Idris Sultan amefunguka na kusema kuwa katika wanawake anaowaogopa Duniani ni wanawake wa marafiki zake na wanawake  wa watu kwaio hawezi kupoita nao hata siku moja na  hata kama atapita nae kama  basi akijua anamwacha.

Idris alifunguka maneno hayo alipokuwa katika kipindi cha kikaangoni live kinachorushwa na EATV,

siku hizi naogopa sana wake za watu maana ukishaona mtu wako wa karibu kanyolewa kipara basi ujue kinachofuata ni kitu kibaya sio kizuri.sijawahi kutoka na mke wa mtu na sijui kama hata ilishawahi kutokea kwa bahati mbaya ila hata mi i sitatak kusikia kuwa kuna mtu katoka na mke wangu alafu kusiwe na msiba kwangu au kwao lazima kuwe na namna ya kuadabishana kwa mambo madogo madogo kama hayo, yaani umetoka na mke wa mtu na mimi natoka na maisha yako.kwaio mimi sitaki kugusa mke wa mtu kwa sababu hata mimi sitaki  kugusiwa wa kwangu.

Idris anasema kuwa pamoja na kwamba hapendi kutoa na wanawake za watu lakini pia hapendi kutoka na wasichana ambao ni ndugu wa jama zake.

download latest music    

girlfriend ni kitu cha kupita tu ni kama kikombe na sahani, kila mtu anaweza kukitumia au kukiacha au labda awe amefanya commitment fulani, na kumchukua kuwa mke hapo tunakuwa tunaongea lugha nyingine tena, ila katika vitu vingine pia ninaogopa ni ma-girlfriend wa marafiki zangu au watu wao wa karibu, hao nawaogopa sana.

Lakini pia katika mazungumzo yake Idris alisem akuwa katika maisha yake ya mapenzi hajawahi kuachwa zaidi ya kuacha.

Idris alishawahi kutoka kimapenzi na mrembo aliewahi kuwa Miss Tanzania Wema Sepetu  lakini mahusiano hayo hayakudumu kwa muda mrefu kutokana na drama nyingi zilizokuwepo katika mahusiano hayo, lakini pia Idris alikiri kuwa Wema anaweza kuwa ndie mwanamke pekee aliekuwa nae katika mahusiano na akawa anajisikia vizuri sana na  ni mwanamke ambae hatoweza kumsahau katika maisha yake pia kwa sababu pia aliweza kumbebea mimba ingawa mimba hiyo iliharibika.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.