Idris Sultan Afungukia Picha Yake Ya Utupu

Comedian maarufu na Muigizaji wa Bongo movie Idris Sultan amefunguka na kuiongelea picha yake ya utupu ambayo ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita.

Picha inayodaiwa kuwa ni Idris imekuwa ikisambaa sana mtandaoni Idris sasa anadai kuwa, ana imani aliyevujisha picha hiyo ni mchumba wake wa zamani na picha hiyo ni ya miaka miwili iliyopita.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris ameandika haya:

Wanaonipenda wanajua mimi mtu wa aina gani, ndugu zangu wanajua mimi mtu wa aina gani, marafiki zangu, mchumba wangu ananifahamu vyema sana, mashabiki wangu wananijua sanaaa hadi wakati mwingine wanajua nini nitasema kabla sijasema. Kampuni zinazonidhamini zinafahamu mimi ni mtu wa aina gani. Hii ndio nguvu niliyo nayo, ni nguvu ya mapenzi”.

Idris anadai kuwa, watu wanaovujisha picha zake mtandaoni ni wenye nia mbaya wanaojaribu kuficha uchafu wao: Sasa ficheni uchafu wenu wa sasa kwa kuweka uchafu wangu wa miaka miwili iliyopita na mwone ni vipi Allah ataendelea kunibariki na mashabiki wangu… Sijutii, ni mitihani tu. Nakusamehe na nakuombea Allah akusamehe pia. Makosa yangu yatabaki kuwa yangu #NguvuYaMapenzi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.