Idris Sultan Alamba Shavu Nono

Muigizaji wa Bongo movie na komedian maarufu Idris Sultan amedaiwa kulamba shavu nono katika ulimwengu wa Burudani Baada ya safari yake ya nchini Afrika ya kusini.

Global Publishers wanaripoti kuwa Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la  Komedi lililoandaliwa na Comedy Central, moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

download latest music    

Mwaliko wa Idris unakuja baada ya mafanikio makubwa katika Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu  ya wapenzi wa comedy hapa nchini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na GPL, Idris alisema lilikuwa na lengo kuu la kuburudisha na kuelimisha watu katika maswala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.

Tarehe 1 Desemba, Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki jijini Dar ambapo watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket. 

Sex Tour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini  Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa  ya muziki”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.