Idris Sultan Ang’ara Zaidi Hadi Marekani

Mshindi wa Big brother mwaka 2014  na mchekeshaji Idris Sultan amepata bahati ya kung’ara ughaibuni baada ya kupata nafasi ya kucheza filamu ya Hollywood nchini Marekani.

Idris amepata nafasi ya kushiriki kwenye filamu hiyo inayoitwa The blue Mauritius iliyoandaliwa na mtendaji mkuu wa kampuni ya D street Media group iliyopo Marekani.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Idris alisema kuwa alikutana na Mmarekani Dexter kwenye maonyesho ya filamu ya kimataifa ya Zanzibar (ZIFF)

” Alivutiwa kufanya kazi na mimi baada ya kuona ushiriki wangu kwenye filamu ya ‘Balling on the others’ tulikutana kwenye tamasha la ZIFF ambalo pia mimi nilikuwepo pamoja na washiriki wenzangu.

Filamu hiyo inatarajiwa kuwa na wasanii wakubwa wa filamu duniani kama Eric Dame Muigizaji Mmarekani, Gerard Depardies Mfaransa na Thomas Kretschmann wa Ujerumani.

Filamu hiyo inatarajiwa kuanzwa kutengenezwa machi  2018, itasambazwa katika majumba makubwa ya sinema duniani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.