Idris Sultan Atangaza Ujio Wa Kipindi Chake Azam TV

Mchekeshaji na Muigizaji wa Bongo movie Idris Sultan ametoa habari njema kwa mashabiki zake baada ya kutangaza ujio wa kipindi chake kwenye Tv yako.

Idris alitangaza Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kipindi chake kilichokuwa kinaruka Kwenye ukurasa wake wa YouTube Kitaanza kuonekana rasmi ndani ya Wasafi Tv.

download latest music    

Nakumbuka wakati SIO HABARI ni show ndogo tu. Nilipoanza lengo kuu ilikuwa kujaribu kusema mambo makubwa na mazito ambayo wengi wanayajua, wanayasikia na labda hawataki kuyaongelea au wanaogopa. Haya mazito tuliyadadavua katika lugha nyepesi na ya kufurahisha na ujumbe ulifika. 

Show ilikaa mwezi tu kwenye TV nikaikatisha kwasababu niligundua ni kubwa kuliko nilivyoichora na ilibidi nifanye hivyo ili isianguke. Ilikua ni show nimelenga vijana tu ila kila jumatatu zilikaa familia kuangalia SIO HABARI. Wakubwa kwa wadogo. Haya niliyajua kwenye malalamiko baadhi ya watu wakisema samahani Idris punguza makali ya maneno tunaangalia na wazazi wetu “mnaogopa wazazi wataharibika au ?” Nilisema ila nikagundua nini kimesemwa bila wao kujua.This is not just a show anymore, hii ni sauti ya wengi wasioweza, ni kitu kimoja chenye ukweli mwingi kinachounganisha familia nzima na kumsikiliza mpuuzi mmoja anayetoa la moyoni. Wengi hamkushtukia show iliruka kwa mwezi mmoja tu.I’m proud to say SIO HABARI inarudi, wayyyyyy bigger than it ever was. Ilikuwa ndoto ikawa idea ikawa jaribio na sasa itakuwa a revolution kwenye ufunguaji wa fikra kwa kutumia lugha nyepesi tu “COMEDY”.. Vicheko itakuwa ni “Hahaha ila ni kweli”.. Soon on AZAM“

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.