Idris Sultan Awatolea Povu Zito Watu Wanaosema ‘Amefulia’

Muigizaji na mchekeshaji wa komedi Idris Sultan amewajia juu watu ambao wamekuwa wakimsema kuwa amefulia ambapo ametaja mali zake zote na njia zake zote alizonazo za kuingiza pesa.

Idris aliukwaa umilionea kwa mara ya kwanza mwaka 2014 aliposhinda shindano la Big brother Africa ambapo alipata kiasi cha dola za kimarekani 300,000 ambayo ilikuwa ni sawa na shilingi milioni 500 za Kitanzania.

download latest music    

Lakini miaka michache baada ya kuwa milionea kulikuwa na tetesi za Idris kufulia Tena ambapo alikiri mwenyewe baadae kuwa kutokana na bad investments decisions amepoteza kiasi kikubwa cha hela lakini alidai pesa yake ilikuwepo kiasi.

Lakini siku za hivi karibuni inasemekana kuwa amefulia Tena na inadaiwa hali yake ni mbaya kwa tetesi zilizopita Kwenye mitandao ya kijamii.

Idris amekana taarifa za yeye kufulia na kupitia ukurasa wake wa Instagram amewatolea povu zito watu wanaodai kuwa amefulia:

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.