Idriss Akiri Kuogopwa na Wanawake.

Msanii na mchekeshaji  bongo Idris sultan amefunguka na kuelezea kuwa kwa muda mrefu wanawake warembo bongo  wamekuwa wakimuogopa na kumkwepakuwa nae katika mahusino kwa sababu ya umaarufu wake na kazi yake katika jamii.

Idris anasema kuwa wanawake wengine wenye msimamo wa maisha na wasiokuwa tegemezi wamekuwa wakimuogopa sana kutokana na ukweli kwamba wanao kuwa watakuwa maarufu na kufatwa fatwa na mapaparazi  kutokana na umaarufu alionao mwanaume huyo.

download latest music    

Idris anaongezea kuwa muda mwingine huwa anahisi kuwa kazi yake ya uchekeshaji inaweza kuwa chanzo cha yeye kutokuwa katika mahusiano kwa sababu wanawake wanakuwa wanahisi kama vile anakuwa yupo katika utani wa kuanzisha mahusiano ilhali  muda huo anakuwa makini na anachotaka kukifanya.

kabla hajakutana na wewe anakuwa tayari kaisha ku-judge  kila kitu kiasi kwamba anakuwa tayari amshakufikiria kuwa wewe ni kichaa.wanahisi kuwa sisi comedians hatuko makini katika hilo .wanadhani kuwa sisi hatuwezi kupenda kama wengine  lakini cha ajbau wenzetu huko nje wanapata wanawake wazuri tena pisiii kabisaaa.

Idris ana malizia kwa kusema kuwa yeye kuwa mchekeshaji kuna mfanya ashindwe kupata mwanamke anayemtaka.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.