Inasemekana Kuwa Johari Ni Mjamzito

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kwa Jina la usanii kama Johari anadaiwa kuwa ni mjamzito kwa miezi minne sasa.

Global Publishers wanaripoti kuwa mtu wa karibu wa Msanii huyo amewapa taarifa hizo kwa sasa Johari ameongezeka umbo kwa sababu ya ujauzito alionao ambapo anafurahia kwani ni jambo alilokuwa akilitafuta kwa muda mrefu.

download latest music    

Mmemuona Johari kwa sasa? Ni mjamzito na mwenyewe ana furaha ingawa anaficha sana ili wapambe wasimharibie”.

Baada ya kupata habari nyepesi nyepesi hizo gazeti hilo lili mmvutia way a ili kujua kama taarifa hizo zina ukweli wowote ndipo Johari alipomwaga povu kidogo:

 Sipendi kuzungumzia hayo mambo yangu binafsi, kama mimba ipo mtaiona tu, lakini pia mimi ni mwanamke na umri wangu unaruhusu kuwa na ujauzito hivyo sioni tatizo“.

Johari tayari ni mama wa mtoto mmoja ambaye alimkubali kwa mara ya kwanza Miezi michache iliyopita baada ya kukataa kwa miaka mingi kuwa hana mtoto.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.