Inawezekana Ni Kweli Diamond Na Zari Mapenzi Yameisha

Tunakuwa na furaha sana katika kumbukumbu za sikukuu zetu za kuzaliwa  tena hasa tunapopata salamu za upendo kutoka kwa watu wetu wa karibu, kwa Dunia hii ya sasa ya utandawazi imekuwa ni kawaida kumtakia kheri ya sikukuu ya kuzaliwa mtu wako wa karibu kwa kuweka picha yake katika mitandao ya kijamii kama Facebook , Twitter lakini hasa hasa ni ukurasa wa Instagram ambao watu wengi kwa sasa  wanautumia.

Tarehe 2  October mwaka huu ilikuwa ni siku muhimu kwa msanii Diamond Platinumz kwa sababu alitimizia miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake,katika siku hiyo Diamond alifanya sherehe mfululizo siku tatu(pre-birthday party) akijumuika na baadhi ya ndugu na marafiki zake wa karibu.Lakini bado kunakuwa na utata kwa sababu tangu  kumeanza kwa shamrashamra hizo, mama mzazi wa watoto wa Diamond hajaonyesha muamko wowote wa kufanya lolote katika siku iyo ya kuzaliwa ya mpenzi wake.

download latest music    

Ikiwa ni kama wiki imepita tangu Zari afanye birthday party yake nchini Afrika ya Kusini , Diamond na team yake nzima ya Wasafi walisafiri na kwenda, je hii haikupaswa kutokea hata kwa Diamond ambae amefanya sherehe hii nchini Tanzania, je ni kweli Zari hakuona umuhimu wa kuudhulia sherehe hiyo , na je kama alikuwa amebanwa na kazi nyingi alishindwa kuonyesha upendo na furaha kwa mzazi mwenzie kwa kumpost katika ukurasa wake wa instagram ilhali akiendelea kupost picha zake? haya  ni baadhi ya maswali ambayo mashabiki wamekuwa wakijiuliza, au zile hasira za Diamond kuzaa na Hamisa Mobeto bado hazijaisha.

Ikumbukwe kuwa kusafiri kwa Diamond kwenda Afrika Ya Kusini ilikuwa ni moja ya vithibitisho kuwa wawili hao walishaweka mambo sawa, sasa je nini kinaendelea,hivi karibuni Zari na Diamond walikuwa katika majibizano ya mtandaoni kuhusu kosa la Diamond kuiri katika media kuhusu yeye kuzaa na video queen Hamisa Mobeto ilhali akikiri kuwa alikuwa anatoa hata matumizi kwa siri bila mzazi mwenzie huyo kujua chochote.

Hakuna aliyeamua kuweka wazi mpaka sasa kuhusu mahusiano yao, lakini kwa kuwa Diamond ni msanii na ana mashabiki pia, mashabiki wamekuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua nini kinaendelea kati ya wazazi hao wawili ambao tayari walishaanzisha familia inayowahitaji sana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.