Irene Akanusha Kupewa Talaka na Dogo Janja.

Mwanadada Irene Uwoya anasema kuwa pamoja na yote yaliyowahi kutokea katika mahusiano yake na mume wake na kufikia hatua ya kuachana kabisa lakini bado amekuwa alimpenda na kumkumbuka sana mpenzi wake.

Wawili hao waliofunga ndoa mwishoni mwa mwaka  jana , walifikia tamati ya mahusiano yao baada ya wawili hao kushindwana ndani ya nyumba kwa sababu za usaliti  huku Dogo janja akionekana ndio mkosaji mkuu na kufanya kila mtu kuanza maisha yake.

download latest music    

Hata hivyo baada ya kuachana kwao, Irene amekuwa msemaji sana katika mitandao na vyombo vya habari kila anapohijiwa kuhusu swala hilo huku akikana kuwa hakuwahi kubadili dini ili kuolewa na mwanaume huyio na kusema kuwa hakuwahi pia kupewa talaka.

hata hivyo irene anasema ” sijawahi kupewa tala na dogo janaja na sijawahi kuacha kumpedna hata siku moja lakini kuna mambo mengine lazima maisha yaendelee,  na ndio maana nikasema kuwa sasa hivi niko busy kufanikisha baadhi ya ndoto zangu nilizokuwa nimejiwekea, mambo ya kuolewa nadhani tuwaachie wengine tu”

Hata hivyo irene anasema kuhusu utajiri wake, watu wengi wamekuwa na tabia ya kufuatilia mtu anafanya nini au uanapata wapi ela  bila kujua kuwa kuna wakati unaamua kufanya mambo kimya kimya na baadae yananyooka wanaanza kushangaa.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.