Irene Ana Mwili Mkubwa ila Umri Mdogo, Wanaendana na Janjarao :-khadija Kopa

Mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini Khadija Omar Koppa, amewakingia kifua wanandoa wawili kutoka tasnia ya sanaa ya bongo, Irene Uwoya na Dogo Janja, na kusema kwamba wawili hao wanastahili kuwa pamoja.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Khadija Kopa amesema kitendo cha watu kumuona Dogo Janja ni mdogo kwa Irene Uwoya si kweli, kwani hata Irene Uwoya ni mdogo isipokuwa ana mwili mkubwa.

download latest music    

Mbona nyie Irene na Dogo Janja mnawaonea sana!? Hivi yule Irene nyie mnamuona mkubwa sana kwa sababu ya ule mwili!? Wala si mkubwa yule mtoto mdogo yule wa juzi, yule Dogo Janja kimwili chake kidogo dogo, ndio kampita lakini sio wa hivyo, lakini vilevile yule si mdogo, mdogo kwa mama yake ndio mwenye kujua kadi yake ya clinic iko wapi, na alokuwa anampeleka kupiga sindano, kwa Irene sio mdogo yule, yule mtu mzima kashaacha shule na mambo yake yapo kama kawaida”, amesema Khadija Kopa.
Khadija Kopa ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha Dogo Janja kumuoa Irene Uwoya sio ajabu kwani hata Mtume Mohamad kwenye imani ya dini ya Kiislam, alioa mwanamke aliyemzidi umri.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.