Irene Paul Azidi Kumwagia Sifa Zari

Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul amezidi kumiminia sifa Zarinah Hassan ‘Zari’ na kudai mrembo huyo anajua kutengeneza jina lake na pia anajua kufanya biashara.

Irene Paul amewataka wasanii wenzake waache kumuonea wivu Zari kwa Dili alilolipata la Softcare na badala yake wajiulize wanafanya nini ili hata kampuni kubwa ziwaangalie wao wanawake Kwanza.

download latest music    

Lakini pia Irene amedai kuwa Zari ni staa mkubwa sio tu nje ya Bongo bali hata nchini kwetu na kudai hajaona bado hajamfikia kwa uwezo wake wa kuweza kuwa kiwango cha juu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Irene alizidi kumiminia sifa hizo Zari na kusema yafuatayo:

Ni staa mkubwa, anajua kumaintain jina lake, simuoni staa wa kumshinda yeye Bongo”.

Wiki iliyopita Zari alipata dili na kampuni ya Softcare kwa ajili ya kuwa balozi wa bidhaa zao za pampasi kitendo kilichowakera watu wengi baada ya kampuni hiyo kumpa dili hilo Mganda wakati kuna Madura staa wa kibongo kibao wangeweza kuwa mabalozi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.