Irene Uwoya Kuolewa Tena Kwa Mara Ya Pili

Malkia wa filamu za bongo Movies  ambae anaingia kwenye orodha ya wanawake wenye mvuto  kwa wasanii  wa kike Tanzania, amezua gumzo mtandaoni baada ya kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram akionekana amevaa nguo ya harusi(shera) .Gumzo ilo linaunganishwa na baadhi ya matukio ya picha za mwanadada huyo siku chache zilizopita alipoweka picha ya pete na kuandika “i cant wait…”, lakini baada ya hapo aliaweka picha nyingine zinazomuonyesha akiwa amevaa shela la harusi.

Katika post hiyo Irene aliandika”pre-wedding with family and friends..my friday will be super than ever….. kuna wakati  tunanyang’anywa tuvihisivyo vizuri kwetu,na kuletewa bora zaidi, ili tujifunze na kuthamini maradufu..asante kwa hili MUNGU”

download latest music    

Kuna baadhi ya watu wameonekana kuwa na wasiwasi na kusema kuwa inawezekana ikawa ni project mpya ya movie inayokuja kwa sababu wamekuwa na mashaka ya kuolewa kimya kimya kwa msanii huyo ingawa kwa sasa imekuwa kama fashion kwa baadhi ya watu maarufu kufunga ndoa zao kimyakimya , na kupost picha tu.

Hii itakuwa ni kwa mara ya pili Irene Uwoya kufunga ndoa, mara ya kwanza alifunga ndoa na mcheza mpira maarufu  kutoka Rwanda Hamad Kataut Ndikumana ambapo walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume lakini baadae walikuja kuachana bila sababu ya kuachana kwao kuwekwa wazi.

Inawezekana Irene hasiwe msanii wa kwanza kufunga ndoa zaidi ya mara moja na kushindwa kukaa na kudumu katika ndoa, au in awezekana pia sasa ikawa ndio uamuzi wake wa kuolewa umefika, wasanii wengi wamekuwa hawadumu katika ndoa na mahusiano yao labda kwa sababu ya kuwa na scandal nyingi kutokana na umaarufu mkubwa walionao.Ingawa pia wapo wanaopiga picha za harusi kwa sababu tu ya kufanya project fulani ya kazi yake ,hivyo Irene Uwoya anatakiwa aandike na kuongelea swala hilo ili kuwatoa kimasomaso mashabiki zake ambao wamekuwa na hamu kubwa kujua juu ya picha hizo.Kama kweli amefunga ndoa basi Kila lenye kheri kwake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.