Irene Uwoya: Wanawake Jamani Acheni Roho Mbaya

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amewatolea povu zito marafiki wa kike ambao amedai kuwa ni marafiki wanafki.

Siku za hivi karibuni Irene amekuwa akitengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii kuanzia uhusiano wake na ndoa yake na Msanii Dogo Janja lakini pia stori ya mgahawa wake pia imekuwa ikivuma ambapo ametuhumiwa kutowalipa wafanyakazi wake.

download latest music    

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Irene Uwoya aliwatolea povu hilo marafiki wote wa kike ambao amedai kuwa ni wanafki;

Hivi kwanini wanawake tunakuwa hatupendani??? Yaani tunajiulizaga sana…badala sisi tushirikiane ndio kwanza tunarudishana nyuma…yaani unamsikia mtu kabisa anakuponda alafu mbaya zaidi hajawahi hata kugombana nae na pengine unamsaidiaga tu Sanaa…yaani unashangaa wanaokuunga mkono ni wanaume badala ya wanawake wenzako….afu ukifanya mabaya ndio wanakusifia balaa ili uendelee kuharibu …afu sasa yeye akifanya yake anataka umuunge mkono anasahau yeye hakuwahi kufanya hivyo yaani kuna mijitu ina roho daaah!!! Mimi sahivi nimeamua si sapoti mtu yoyote asiye ni sapoti…na haina haja ya kuleana kabisa mtu asiyekuwa na umuhimu kwenye maisha yako atakurudisha nyuma tu! Achana na watu wasio na faida wala mchango wowote kwenye maisha yako….badilika achana na marafiki wanaokushauri starehe siku zote….kaa fikiria katika hao rafiki zako kuna siku hata moja walikushauri kitu cha maana cha kuingiza pesa??? au bata tu? Punguza watu wasio na mashko kwenye maisha yako..Punguza marafiki wasio na faida!!!”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.