Jackline Wolper Ampa Shavu Harmonize

Kwa jinsi ambavyo Wolper na Harmonize walivyokuwa wakitupiaa maneno katika mitandao ya kijamii inakuwa ni vigumu kuamini kuwa leo hii Wolper anaweza kumsapoti Harmonize kwa kitu chochote, lakini hali imekuwa tofauti kwa mwanadada huo ambae ni msanii mkubwa wa tasnia ya filamu nchini lakini pia kwa sasa amekuwa akijihusisha na ujasiriamali wa nguo  jijini bongo.

Katika ukurasa wake wa instagram jana oktoba 17, Wolper ameshangaza mashabaiki wake wengi na kuwaacha na butwaa  baada ya kuposti video zaidi ya tatu ambazo zinamuonyesha akiimba na kucheza wimbo mpya wa mpenzi wake huyo wa zamani Harmonize wimbo ambao unaitwa Shulala, aliomshirikisha Koredo Bello msanii kutoka Nigeria huku chini akiandika caption ya kumsifia msanii huyo kuwa kibao icho ni kizuri,

download latest music    

haka kanyimbo kazuri sana  na video ndo usiseme!!Raaaj bhana umejua kunyoosha, kama bado ujaangalia video ya haka kawimbo pita  kwenye bio ya @harmonize _tz. #uliyemchokozakaja #shulala #naukinibipuTuNakupigia.” aliandika Jackline Wolper

Kitu cha kuhoji na kinachowashangaza wengi ni kwamba juzi tu zilivuja meseji zikionyesha Wolper akimwambia Sarah ambae ndie mpenzi mpya wa msanii huyo kuwa kama amemshindwa Harmonize  basi amuache yeye amrudie kwaio mashabiki wengi wameanza kutoa majawabu kuwa inawezekana Wolper kaamua kufanya kweli na kumrudia Harmonize.

Jackline Wolper na Harmonize ni moja ya couple iliyo-trend sana mjini kipindi cha nyuma na kuwaaacha watu wengi midomo wazi wa sababu Harmonize alikuwa na umri mdogo kuliko Jacky, lakini kutokana na mapezi waliosema kuwa nayo hawakuona tofauti yeyote,baadae Jackline na  Harmonize walikuja kutengana na kusababisha wawili hao kutupiana maneno ya matusi mitandaoni.,huku sababu ya kuachana kwa wawili hao ikitajwa kuwa ni baada ya Harmonize kupata mwanamke mwingine wa kizungu ambae alikuwa akimpa ela nyingi Harmonize.

Ugomvi wa Harmonize na Wolper ulisababisha mpaka Harmonize kuingia studio na kumtungi Jacky wimbo ambao uliongea mambo mengi yaliyohusu mahusiano yao yaliyopita, ukiachia hapo Sarah ambae ni mwanamke wa Harmonize pia alikuwa akigombana sana na Jacky kwa sababu ya Harmonize.Hata hivyo Jacky ndo kashaamua kumpa shavu Harmonize , hatujui kama ni kiki au anataka tu kumuumiza roho mwanamke mwenzie.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.