Jacqueline Wolper aamua kurudi shule baada ya Jux kuitimu masomo yake nchini China

Juma Mussa maarufu kama Jux ameitimu masomo yake nchini China. Msanii huyo amepata shahada ya Computer Science aliyosomea kwa muda wa miaka minne.

Jacqueline Wolper amepata changamoto ya kurudi shuleni baada ya kuona picha ya Jux akisherekea baada ya kuitimu masomo yake nchini China.

download latest music    

“Nimekumbuka mbali kweli nilivyoiona hii picha, nakumbuka siku hizo mwenyewe ndo nakupeleka airport unaenda kuanza kusoma mpaka na mimi nilitamani kuwa mwanafunzi ili twende wote yaani naandika hii caption huku nasmile nikikumbuka hiyo siku ndo unaenda kusoma mwenyewe…am very happy for you mwanafunzi wangu! yani verrrrry happy…! Hongera sana siku hizi vijana wanafanya yote na shule ipooo ndo unazidi kuwa mnyamweezi, mimi mwenyewe hapa nataka nirudi shule ya kutafuta hela manake maisha magumu sana… Hongera sana kwa kuhitimu..!!nisaidieni kumtag mwanafunzi wangu,” Wolper aliandika.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere