Jacqueline Wolper: Nimepoteza Muda Wangu Mwingi Kufanya Bongo Movie

Muigizaji maarufu wa Bongo movie ambaye hivi sasa amegeuka na kuwa mjasiriamali Jacqueline Wolper ameeleza majuto yake ya kupoteza miaka mingi ya kufanya Sanaa ya Bongo movie.

Wolper amekuwa maarufu Kwenye tasnia ya Bongo movie kutokana na filamu kadhaa alizoigiza kuanzia miaka ya nyuma huko tangu enzi za supastaa marehemu Kanumba.

download latest music    

Miaka ya hivi karibuni upepo umebadilika na kumekuwa na maneno kadhaa ya kuelezea kifo cha Bongo movie huku wadau wengi wa filamu wakilia na suala la hatimiliki kuua soko la Bongo movie lakini watu wengi hasa mashabiki wameongelea suala la ukosefu wa ubunifu na uhalisia kuua soko.

Wolper amefunguka na kusema anajutia kupoteza muda wake kukomaa na Kufanya Bongo movie kwa miaka yote badala yake anaona angejiingiza kwenye ushonaji kama hivi sasa. Wolper anamiliki duka la nguo ‘Boutique’ linalojulikana kama Wolper house of stylish.

Wolper ameongea hayo na Global Publishers ambapo amedai kuwa miaka kumi iliyopita alitumia nguvu kubwa mno kukuza jina lake kupitia sanaa lakini ukweli ni kwamba angetumia nguvu hiyo kukuza kipaji chake cha ushonaji basi bila shaka angekuwa mbali:

Ningejua tangu mwanzo ningekomaa na mitindo maana naona huku watu wananielewa zaidi na ninapata pesa nyingi lakini kwenye filamu nimeishia kujulikana”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.