Jay Moe- Muziki Umekuwa Biashara

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Jay Moe aliyejipatia umaarufu kipindi cha nyuma kwa staili yake ya kipekee ya kuchana amefunguka na kudai kuwa hivi sasa muziki umekuwa biashara.

Jay Moe amedai kwa sasa kuna vitu vingi ambayo vimebadilika kutoka wa wasanii wa muziki wa hip hop kutoka na muziki kubadilika na kuwa biashara tofauti na zamani.

download latest music    

Jay Moe alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Ladha 3600 cha EFM ambapo alifunguka haya ziadi:

Sasa hivi tunawekeza sana kwenye muziki tofauti na miaka ya zamani tunatoa wimbo tu hakuna uwekezaji wowote ambao tulikuwa tunaweka.

Lakini sasa hivi au miaka ya sasa hivi muziki umekuwa biashara, kwahiyo lazima pia unavyowekeza uhakikishe uwe na target nzuri ya kuweza kujua pesa yangu itarudi vipi”.

Tofauti na miaka ya nyuma wakati Wakina Jay Moe na wasanii wengine wakongwe wanaanza muziki ulikuwa haujapewa nafasi kubwa kiasi hicho lakini sasa mambo yamebadilika na muziki unaendesha maisha ya watu wengi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.